Lutheran Radio Centre

 

Travel Report Vudee Same

 

March 8th  and 15th March 2012

Participants:  Deo Mosha,Zawadi Mchome

                      Na dereva Temba Inyasi

 Mita ya umeme wa   Tanesco kanisani,ikizunguka kwa kazi kutokana na matumizi makubwa

 

Milima ya Vudee

 

 

 

 

 

Baadhi ya vifaa vinavyohitaji matengenezo

Mitambo iko hewani baada ya matengenezo

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

   Hali ya mnara inahitaji uangalizi(supporting wire)

Nyasi ndogo ndogo zinazozunguka mnara ni hatari moto unapotokea

 

 

    Sehemu ya kitasa      kilichoharibika

 

Baada ya matengenezo

 

Lipo tatizo la wakazi/wenyeji kuchoma msitu moto ni hatari kwa eneo mitambo

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

ü     Tuliondoka Studio saa tatu asubuhi

tulifika Vudee saa tano na nusu, tulipita kanisani kusoma mita yetu ya umeme na ilionekana kuna matumizi makubwa ya umeme yasiyo ya kawaida

 

ü     Kisha tulielekea nyumbani kwa Mzee Mzava mahali ambapo umeme unaanzia kuelekea mlimani kutokea kanisani.

 

ü     Kwanza tuliuliza maswali mbalimbali ili kupata picha nini kimetokea hadi umeme/mitambo kuzima,

ü     Moja ya sababu tulizopewa ni short ya wire iliyosababishwa na wezi wa umeme.

 

ü     Baada ya kusikia mengi toka kwa mzee mzava niliamua kuanza kuangalia mahali ambapo wire unafika toka katika mita kanisani,hapa niligundua uunganishaji mbovu wa wire mbalimbali nah ii ilikua sababu ya kwanza ya short,hapa tulirekebisha kazi iliyochukua zaidi ya masaa matatu,kwa bahati mbaya umeme wa Tanesco ulikatika na kukwamisha kazi ya kuendelea mbele kutafuta sehemu nyingine yenye tatizo.

 

ü     Tulisubiri umeme kurudi  bila mafanikio na hivyo kuamua kutumia mita yetu kupima sehemu mbalimbali kuelekea mlimani kazi iliyokwamishwa na giza na hivyo kuamua kusitisha zoezi husika.

 

ü     Kutokana na umbali kufika Vudee kutokea Moshi tuliamua kutafuta fundi kijijini ili kuendelea na kazi siku iliyofuata na hapa tulifanikiwa kumpata fundi kwa makubaliano akimaliza kazi alipwe Shs 70,000/=

 

ü     Tuliondoka Vudee saa kumi na mbili na nusu jioni kurejea Moshi na kufika Studio saa tatu na nusu usiku.

 

 

 

 

 

 

 

15th March 2012.

ü     Tuliondoka Studio saa tatu na nusu  na kufika Vudee saa  sita mchana.

 

ü     Tulikagua kazi aliyofanya fundi na haikua na matatizo kasha tukaanza safari kuelekea mlimani katika mitambo na kurekebisha fuse box iliyokuwa imeharibiwa na short.

 

ü     Kutokana na mlango kugoma kufunguka tulilazimika kuharibu kitasa na kufunga tena kwa mnyororo na kofuli.

 

ü     Tulishuka toka mlimani na kuanza mazungumzo ya kina juu ya tatizo la wezi wa umeme,na ndipo ilipogundulika kuwa vijana waliokuwa wanatunza mnara na umeme ndio waliohusika na wizi huu kwa kuwauzia majirani wanaoishi jirani na line ya wire na mmoja wa wanaotumia umeme huo isivyo halali ni mtoto wa mzee Mzava jambo lililomsikitisha sana Mzee Mzava mwenyewe.

 

ü     Vijana hawa tayari wametoroka kijijini.

 

Mapendekezo toka Mzee Mzava.

 

1.Wire ihamishwe toka njia ya zamani, hakuna

Usalama,kwani ndiko wezi wanapata mwanya wa

Kuhujumu.

2.Sehemu ya mita 585 iwekwe wire nene ya ardhini.

 

Hasara

1.Tumelazimika kununua wire wa mita 100  kuweka zilizoharibiwa na wezi hao

         2.kumlipa fundi Tsh 70,000 kusaidia kazi ya

Kurekebisha wire

3.Safari mbili kwa watumishi watatu  kufika Vudee.

4.Bill ya Tsh 998,000/=

5.kuharibika kwa mlango wa kuhifadhi mitambo

Iliyogharimu Tsh 34,000/=kuweka kifungio

cha dharura

 

Mafanikio

ü     Radio iko hewani tena baada ya juhudi za watumishi wa Kituo.

 

Mwisho

 

ü     Tulianza safari kurudi Moshi saa kumi na mbili jioni na kufika Studio saa tatu usiku.

 

 

 

 

 

Prepared by Mosha

March 2012.